Masharti ya wachumbatz.com

1.Kujiunga lazima uwe na angalau miaka kumi na nane na kuendelea watoto hawaruhusiwi.
2.Huruhusiwi kuweka picha ya utupu.
3.Huruhusiwi kufungua account zaidi ya moja.
4.Ikiwa utakua na maombi ya uchumba matano na kuendelea wachumbatz.com inaweza kukutumia ujumbe wa kukutaka kuingia kwenye account yako ili kukubali au kukataa maombi ya uchumba.
5.Hakikisha umejiunga bure na umeridhika na huduma ya wachumbatz.com ndipo unaweza kulipia account yako ikiwa hujaridhika tafadhali futa account yako kabla ya kufanya malipo yoyote.
6.Pesa ya kutumia ukisha tuma hairudishwi.
7.Huruhusiwi kuweka matangazo ya biashara , namba ya simu au mawasiliano mengine kwenye sehemu ya profile picha au sehemu ya kuandika kuhusu wewe au kuhusu mchumba unayemtaka .
8.Usipoingia kwenye account yako kwa mda wa mwezi mmoja account yako ya wachumbatz.com itafutwa.
9.Ni wajibu wako kujiridhisha kwamba mtu unayekutana nae na kuanzisha mahusiano ni mtu salama, wachumbatz.com haitahusika na lolote litakalowakuta na huyo mchumba wako baada ya kukutana.
10.Msimamizi wa website hii anaweza kuifuta account yako ukikiuka masharti ya wachumbatz.com pia hatua za kisheria zinaweza kuchukuliwa.
11.Kwakutumia website ya wachumbatz.com unakua umekubaliana na masharti yote ya wachumbatz.com

Mambo ya kuzingatia

1.Hakikisha mtu unayeanzisha naye mahusiano ni mtu salaama.
2.Hakikisha mazingira unayo enda kukutana na mchumba wako baada ya kukubaliana ni salaama.
3.Hakikisha unapoenda kukutana na huyo mchumba wako kwa mara ya kwanza usiende peke yako.
4.Kwa mwanamke au msichana hakikisha unamwambia huyo mchumba wako uliyempata kupitia wachumbatz.com aje mkutane kwenu ajitambulishe kwa wazazi au ndugu na jamaa na ndipo hatua zingine zifuate.
5.Kumbuka ukipata mchumba kabla ya kukutana nae ana kwa ana wajulishe wazazi, ndugu au jamaa zako wa karibu.
6.Unapojiunga na kutumia wachumbatz.com kumbuka kumuomba Mungu na kumshirikisha yeye ili akusaidie kupitia mtandao huu upate mchumba umpendaye na wakukufaa katika maisha ili muishi kwa amani na furaha katika maisha ya ndoa na maisha yako yote.
7.Hakikisha hufanyi tendo la ndoa kabla ya kupima afya zenu na kufunga ndoa na huyo mchumba wako utakaye mpata kupitia wachumbatz.com.

Ushauri

1.Ni wajibu wako kujiridhisha kwamba mtu unayekutana nae na kuanzisha mahusiano ni mtu salama. kumbuka kuweka picha kwenye profile yako itakua rahisi kwako kukubalika na wachumba pindi utakapo tuma maombi ya uchumba kwani mchumba atakua anajua nani anamkubalia uchumba. Lengo la website hii ni kukufanya wewe upate mwenza wa maisha na ni kwaajili ya walio serious tu.
2.Usitume pesa kwa mchumba usiyemjua vizuri! Ukiona umepata mchumba anakwambia umtumie pesa hata hamjaonana ana kwa ana mmekutana tu online( mf. Wachumba Tanzania, instagram, facebook nk) na wala kwao hukujui achana naye mchumba mwenye nia ya kweli hawezi kutanguliza pesa.

Muhimu

Huu ni mtandao pekee ambapo Mwanamke au Msichana anaweza kumuomba uchumba Mwanaume yeyote atakeye mpenda , na pia Mwanume anaweza kumuomba uchumba Mwanamke au Msichana yeyote atakaye mpenda. Kumbuka Kila mtu anayejiunga na Wachumba Tanzania lengo lake ni kutafuta mchumba kwahiyo kua huru kumuomba uchumba yeyote utakaye mpenda. Pia kumbuka huu sio mtandao wa kuchati na kujifurahisha bali ni mtandao maalumu kwa ajili ya kupata mwenza wa maisha na kuepukana na upweke.

Sera ya faragha (Privacy policy)

Taarifa zinazoifadhiwa pindi unapojiunga na baada ya kujiunga na website ya wachumbatz.com
Taarifa zako tunazohifadhi pindi unapojiunga na baada ya kujiunga na website ya wachumbatz.com ni pamoja na jina lako , namba ya simu , umri , pamoja na mkoa unakotoka kama ulivyojaza kwenye fomu,ip, aina ya browser, namba ya siri (password) tunahifadhi katika mfumo maalumu (encryption) ambapo si mfanyakazi wa website ya wachumbatz.com au mtu yeyote anaweza kuijui hivyo hupaswi kumwambia mtu yeyote namba yako ya siri. Picha unaweza kuweka kwenye profile yako baada ya kujiunga na website ya wachumbatz.com.
Jinsi taarifa zako zinavyotumika(How do we use your Personal Information)
Taarifa zako kama jina na namba ya siri ni kwajili ya kuingilia(login) kwenye account yako ya wachumbatz.com , Pia jina , umri , mkoa unakotoka pamoja na picha yako ni kwaajili ya waliojiunga pia kukujua wewe ni nani na uko wapi pindi wanapofanya machaguo ya wachumba , namba ya simu ni kwaajili ya kulipia account yako pindi utakapo hitaji kulipia account yako na pia ni kwaajili ya mawasiliano kati yako na mchumba uliyempata kupitia wachumbatz.com ,namba ya simu , messages, mchumba uliyempata, ulizotumiwa au kutuma zinabaki kuwa siri yako,ip na aina ya browser ni kwaajili ya statistics na security(usalaama) wa mtandao wa Wachumba Tanzania Angalizo : ukimkubali mchumba namba yako ya simu itatumwa kwake na yako itatumwa kwako. Pia kwa wasioweza kutumia huduma hii nakuomba kuugwa na wahudumu wa wachumbatz.com, pindi wanapoungwa wahudumu watakubali maombi ya waliowaomba uchumba moja kwa moja namba simu ya aliyeomba kuungwa itatumwa kwa aliyeomba uchumba.
Security(Ulinzi wa data)
We follow generally accepted industry standards to protect the Personal Information submitted to us, both during transmission and once we receive it (including encryption and password protection).However, no method of transmission over the Internet using industry standard technology is 100% secure. Therefore, we cannot guarantee the absolute security of your information.
Delete Account(kufuta account yako)
Ukifuta account yako ya Wachumba Tanzania au Tukifuta account yako Taarifa zako zote zinafutika ,baadhi ya taarifa kama jina lako namba ya simu na ip zinabaki kwa mda wa siku saba ambapo nazo zitafutika kabisa, Kumbuka ukiacha maoni yako wakati wa kufuta account yako picha ya profile jina umri pamoja na maoni/ushuuda vitaonekana sehemu ya maoni/ushuuda.
Disclose Personal Information(Utoaji wa taarifa binafsi)
We may disclose Personal Information to government of United Republic of Tanzania third parties, including government regulatory bodies and law enforcement as required, authorised or permitted by law.
Mabadiliko ya Sera ya faragha(Changes to our Privacy Policy)
Tunaweza kubadili(change or update) Sera ya faragha mda wowote tunakushauri kutembelea ukurasa huu mara kwa mara.